Serikali Wilayani Nkasi, Rukwa imeagiza kukamatwa kwa wazazi wa mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi mkinga kwa kosa la kuandaa mpango wa kumuoza mwanafunzi huyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda alitoa agizo hilo jana, amesema;

”Naagiza wazazi wote wa mwanafunzi huyo wakamtwe mara moja na aliyempa mimba afikishwe katika vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake”

Mtanda ameongezea kuwa tatizo la mimba wilayani hapo bado ni kubwa kwani miezi iliyopita wanafunzi 27 walipata ujauzito.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri, Misana Kwangula amesema lengo la serikali kugawa pikipiki kwa waratibu wa elimu kata ni kuwawezesha kutembelea shule zilizopo katika kata zao.

Aidha amewataka waratibu wa elimu kata kutambua majukumu yao na kuhakikisha wanatokomeza mimba mashuleni hasa hawa wa elimu ya msingi.

Watakaoshiriki fainali za U17 wafahamika rasmi
CAF yamsafisha Jerry Yekeh

Comments

comments