Katika mahusiano kuna mambo mengi ambayo yanatokea mengi ni yale yatarajiwayo na mengine ni yale yasiyotarajiwa.

Huko London mwanaume mmoja anayejulikana kama Simon Louis (49) amekataliwa ombi lake na mpenzi wake  la kumuoa Mary Emmanuella (41)  ambaye ni mpenzi wake aliyempenda mpaka kuokoa maisha yake mara baada ya kujitolea figo yake kumpandikizia na kunusru maisha yake pindi figo zake kufeli na kukaa coma kwa muda wa miezi miwili.

Hata hivyo Simon alipohojiwa na chombo cha habari cha Metro UK alisema kuwa hajutii maamuzi yake ya kumpa figo mwanamke huyo aliyempenda hata mara baada ya kukataa ombi lake alipopona ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa figo.

”Nilimpa moyo wangu, lakini pia nilijifikiria nikampa na figo yangu, chochote kilichotokea sijutii wala sitojutia kwa kumpa zawadi ya maisha” amesema Simon.

Aidha Mary Emmanuella amesema ataendelea kuwa rafiki wa karibu wa Simon.

Ni rafiki angu sana na daima itakuwa hivyo, mapenzi kati yetu ni ya kweli, Simon angefariki kwa kile alichokifanya kwa ajili yangu” amesema Simon.

Kwa mara ya kwanza wapenzi hao walikutana Club mnamo mwaka 1990 pindi Simon akiwa na umri wa miaka 28 huku Mary akiwa na umri wa miaka 20.

Mnamo Septemba 2014 Mary akiwa na miaka 37, gafla alianguka na ngozi yake kugeuka kuwa njano, mwanae Dwayne alimkuta chini akiwa anatapika na kumkimbiza hospitali huko London ambapo alikutwa na ugonjwa wa figo uliofikia hatua mbaya na njia pekee kuokoa maisha yake ilikuwa ni kupandikiza figo nyingine.

 

 

 

 

Juan Cuadrado akubali yaishe kwa Ronaldo
Lugola alivyotofautiana na Mzee wa Upako

Comments

comments