Hafla ya kumuapisha Lazarus Chakwera kuwa rais mpya wa Malawi imefanyika leo, June, 28,2020 katika mji mkuu wa Lilongwe baada ya kiongozi huyo kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.

Chakewera alimshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Peter Mutharika kwa asilimia 58.57 ya kura katika uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.

Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, kushangilia ushindi huku baadhi wakipiga honi za gari na wengine kufyatua fataki.

Jana, Jumamosi, Mutharika alizungumza na kusema kuwa ingawa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi, ni imani yake kwamba nchi inastahili kusonga mbele.

Ikumbukwe kuwa, Malawi ni nchi ya kwanza Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuandaa duru ya pili ambayo upinzani ukanyakua ushindi.

Habari picha: Rais Magufuli akizindua mradi wa maji Kisarawe
Zimbabwe yasitisha miamala ya fedha kwa simu