Kundi la kigaidi linalojiita Islamic State limeachia video inavyomuonesha mtu ambaye ameelezwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo akikiri kupigwa huku akiahidi kulipa kisasi.

Abu-Bakr al-Baghdadi, ameonekana kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014 alipoonekana kwenye kipande cha video akiwa Mosul, alipotangaza kuanzishwa kwa oparesheni za kundi hilo katika maeneo ya Syria na Iraq. Baghdadi alikuwa ameripotiwa mara kadhaa kuwa ameuawa na majeshi ya Marekani na washirika wake.

Katika kipande hicho cha video iliyowekwa kwenye mtandao wa kutoa habari wa kundi hilo unaoitwa al-Furqan ikielezwa kurekodiwa mwezi huu, Baghdadi ameeleza kuwa anafahamu kundi hilo limeshindwa katika vita huko Baghuz ambako ndiko ngome kuu ya kundi hilo lakini wanajipanga upya kwa ajili ya kulipiza kisasi.

Katika video hiyo, Baghdadi amedai kuwa mashambulizi yaliyofanyika Jumapili ya Pasaka nchini Sri Lanka yalikuwa na lengo la kulipa kisasi kwa kuondoshwa kwenye ngome yao ya Baguz iliyoko nchini Syria.

Msemaji wa Idara ya Marekani, amekaririwa akieleza kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu video hiyo ili kufahamu uhalisia wake na kwamba watahakikisha kila kiongozi wa IS aliyosalia wanakutana na mkono wa sheria kadiri wanavyostahili.

Hii ni ajabu kweli, unafungwa uko nyumbani?- JPM
Marekani: Naibu Mwanasheria Mkuu ajiuzulu, amuandikia Trump ujumbe