Katibu Mkuu mastaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema baada ya kufanya kazi za siasa muda mrefu, sasa ni wakati muafaka kwake kuanza kufundisha vijana vyuoni juu ya uongozi.

Amesema anatamani mambo yote aliyojifunza katika maisha yake ya uongozi serikalini na nadani ya chama hicho ayarithishe kwa vijana.

Amebainisha hayo alipo ongea na Nipashe, na kuongeza kuwa mambo mengi ambayo amejifunza hayapo kwenye vitabu bali yanapatikana kwenye utendaji.

“Katika maisha yangu ya uongozi na hasa maisha yangu ya utendaji serikalini na ndani ya chama, nimejifunza mengi na nimekutana na mambo mengi nimepata fursa ya kujifunza mambo mengi na pia nimeweza kuwa mwanafunzi wa vitendo” Amesema Kinana.

Na kuongeza kuwa ” Kila unapozunguka unaona mengi na unajifunza mengi kwa hiyo ninatarajia kuendelea kutoa mchango wangu katika uzoefu wangu kwenye uongozi, ninatarajia na tayari nimepeleka maombi kwenye vyuo mbalimbali, na baadhi ya vyuo vimekubali nitoe mafunzo hasa katika masuala ya uongozi”

Aidha amebainisha kuwa uongozi una mambo mengi likiwamo suala la uvumilivu na kuwa karibu na watu, kuwa mkweli, msiri na pia umuhimu wa kusoma, tena kusoma sana.

Mkwasa afunguka ripoti ya vipimo
Tetesi za usajili barani Ulaya