Kanye West amemshtua mkewe Kim Kardashian baada ya kumwambia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuwa anataka kuwa na watoto saba.

Kanye West alijibu swali la Rais Museveni ambaye alitaka kujua ana watoto wangapi, alipotembelea ikulu ya nchi hiyo akiwa na mkewe pamoja na mtoto wao North West.

“Nina watoto watatu, lakini ningependa kuwa na watoto saba,” alijibu Kanye West.

Hata hivyo, kamera zilipoelekezwa kwa Kim K, zilionesha sura ya kupinga mpango huo huku akitikisa kichwa kumaanisha kuwa ‘nisingependa kuwa na watoto saba’.

Wawili hao wana watoto watatu ambao ni North (5), Saint (2) na Chicago (miezi 10).

Kim alijifungua kwa njia ya kawaida wanaye North na Saint, lakini alipata changamoto za kiafya katika muda wa ujauzito pamoja na kujifungua.

“Mama yangu alikuwa analia, hakuwahi kuona kitu kama hiki kabla. Kujifungua kwangu kulikuwa rahisi, lakini nilipitia changamoto nyingi za kiafya. Hali ya maumivu zaidi niliyowahi kuyapata kwenye maisha yangu,” Kim K aliwahi kusema.

Gekul: Chadema hangaikeni kujibu hoja zangu
Serikali yasimamisha huduma hospitali za Marie Stopes

Comments

comments