Mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina la Hassan Mtiko (49) amejiua kwa sumu, muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kumhukumu kifungo cha miaka 60 jela kwa makosa ya ubakaji na ulawati.

Mtiko alikutwa na hatia ya kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kumzaa katika eneo la Dorcas mjini Hai mkoani Kilimanjaro na kumhukumu miaka 30 jela kwa kila kosa, hivyo kutakiwa kutumikia miaka 60 jela.

Mtiko amedaiwa kunywa sumu juzi akiwa katika mahabusu ya kituo cha polisi cha Bomang’ombe mjini Hai alipokuwa akisuburia kupelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo alichopewa.

Kwa mujibu wa Mwananchi, Chanzo chake kimeeleza kuwa Mtiko aliwaomba askari kumruhusu kwenda chooni na kwamba alipotoka huko hali yake ilionekana kuwa mbaya. Mahabusu waliripoti kwa askari tukio hilo ndipo alipokimbizwa hospitalini ambapo alilazwa na baadae kufariki.

Kaka wa Marehemu, Hassan Jumanne Mtiko alithibitisha kuwa ndugu yake alifariki mikononi mwake alipokuwa akimuuguza baada ya kunywa sumu akiwa mahabusu.

“Sasa hivi tumemhifadi kwenye chumba cha maiti,” kaka wa marehemu anakaririwa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa hakuweza kutoa taarifa juu ya tukio hilo jana baada ya kuwaeleza wana habari kuwa alikuwa kwenye kikao.

 

Simba SC Watangaza Dau La Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
Wabunge CUF wafichua ‘njama’ inayosukwa na Lipumba