Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa alianza shughuli za kilimo na ufugaji tangu mwaka 1988, na kuongeza kuwa kama kuna mtu anasubiri kustaafu ndipo aanze shughuli hizo atakuwa amechelewa.
 
Amesema kuwa matarajio yake kwa sasa ni kuongeza ng’ombe wa maziwa 500, hivyo amewataka wafugaji kufuga kisasa ili waweze kufaidika na kupata soko la uhakika kulingana na bidhaa bora watakayokuwa wanaitoa.
 
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kijiji kwake Msoga mkoa wa Pwani, ambapo ameongeza kuwa kazi hiyo ya ufugaji na kilimo mara nyingi huwa inachangamoto kubwa pindi umri unapokuwa umeenda.
 
“Ukishazeeka ndio uanze kufuga ama kulima? ukikuta mtu anasubiri kuzeeka au kustaafu ndipo aanze kazi hizi za ufugaji na kilimo, basi ujue huyo kachelewa, mimi nilianza kufuga tangu nikiwa waziri,”amesema Dkt. Kikwete   
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa alianza shughuli za ufugaji akiwa na ng’ombe 40, ambapo kwa sasa anamiliki za ya ng’ombe 400 kijijini kwake Msoga.

Galatasaray Kubisha Hodi Kaskazini Mwa London
Hili ni jibu la Ali Kiba kwa ‘Diss’ ya Diamond? ‘Najua unanichukia…’