Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye leo asubuhi alikuwa miongoni mwa wageni waliotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kwa lengo la kushuhudia kiapo cha mkewe mama Salma kama Mbunge, amesema neno kuhusu nafasi hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Dkt. Kikwete ambaye utambulisho wake uliwainua wabunge wote wakimshangilia bila kujali itikadi zao za vyama, amesema kuwa huu ni wakati wa yeye kumuunga mkono mkewe.

“Leo asubuhi nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga mkono,” alitweet.

Mama Salma Kikwete

Bi. Salma Kikwete aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mbunge akiweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza aliyewahi kuwa ‘First Lady’ kuingia Bungeni kama muwakilishi wa wananchi.

Kuonesha jinsi alivyo tayari kwa kazi hiyo, leo ameweza kuuliza swali lake la kwanza ambapo alitaka kujua kuhusu huduma za TASAF katika mkoa wa Lindi. Swali lililojibiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki.

LIVE: Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
Tottenham Hotspurs Kuivurugia Crystal Palace