Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza kufurahishwa na hatua ya msanii Hamisi ‘Mwana FA’ Mwinjuma kuufanyia kazi ushauri aliowahi kumpatia miaka kadhaa iliyopita.

Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mtu wa karibu wa wasanii akiwaalika mara kadhaa Ikulu na kushiriki nao kwenye hafla mbalimbali, ameeleza kufurahishwa na namna ambavyo Mwana FA ametambulisha bidhaa yake mpya ya ‘Body Spray’, akieleza kuwa aliwahi kumshauri kutojikita kwenye kazi moja tu ya muziki.

“Kuna siku nilimsihi @MwanaFA na wanamuziki wengine kufanya shughuli nyingine zaidi ya muziki pekee. Nimefarijika leo kunitembelea na kutambulisha bidhaa yake mpya ya “body spray”. Hii ni hatua kubwa na nzuri kwa vijana wetu. Tuwaungishe!” Dkt. Kikwete ametweet.

Mwana FA alizindua bidhaa hiyo wiki hii, ambapo ameibatiza jina la ‘Fyn by Falsafa’.

Mbali na Vanessa, msanii mwingine ambaye ametambulisha bidhaa yake wiki hii ni Vanessa Mdee, ambaye ameshirikiana na kampuni moja kutambulisha biashara yake ya kuuza viatu vya wanafunzi wa kike alivyoviita ‘Bora Star‘.

LIVE: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Salenda
Masha ataja siku ya kuingiza ndege tatu mpya za Fastjet, ‘wiki hii…’

Comments

comments