Baada ya Jeshi la Polisi nchini kutangaza kuwakamata wanawake watatu ambao walikuwa wakitumia majina ya Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na mkewe kwa kuiba fedha za wananchi kwa kuwalaghai kuwa wanatoa mikopo kupitia Vicoba kwa njia ya mtandao wa facebook, Kikwete ameibuka na kulipongeza jeshi la Polisi.

“Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa” amesema Jakaya Kikwete

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Polepole azidi kuwang'oa upinzani
Ashikiliwa na Polisi kwa kughushi nyaraka za Serikali