Mwanamke mmoja nchini Jamaica anayedhaniwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani, Violet Mos Brown amefariki akiwa na umri wa miaka 117.

Katika taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamaica kupitia ukurasa wake Twitter imesema kuwa mwanamke huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 117 kitu ambacho ni adimu kufikia umri huo kwa sasa.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimesema kuwa kikongwe huyo amefariki katika hospitali moja iliyopo katika mji wa Montego Bay na inadhaniwa kuwa ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani.

Aidha, Violet Moss Brown, alizaliwa mwaka 1900 na katika uhai wake alikuwa akila chakula cha aina yeyote lakini hakuwahi kula nyama ya nguruwe na kuku ambayo ilikuwa ni mwiko kwake.

Hawa ndio mashabiki wa muziki wa Jux
Rooney kupokelewa kama mfalme Old Trafford

Comments

comments