Kijana wa miaka 17 amepofuka macho kwa ulaji wa vibanzi (chips) na mkate mweupe, imeelezwa kuwa tokea alipokuwa shule ya msingi alikuwa hali vyakula vya aina nyingine hali iliyompelekea kupoteza uwezo wa kuona.

Utafiti uliochapishwa katika Jarida la tiba nchini Uingereza na kuwekwa kwenye mtandao wa CNN, wanasayansi kutoka chuo Kikuu cha Bristol  wamethibitisha kumchunguza mgonjwa huyo ambaye amekuwa na tabia ya kuchagua vyakula.

Aidha, kijana huyo alimwambia daktari kuwa amekuwa anakula vibanzi (chipsi) vya mtaani, mikate, soseji na nyama nyembamba tangu anasoma shule ya msingi na kwamba alikuwa hali vyakula vya aina nyingine tofauti.

Kwa mujibu wa andiko lililochapishwa Jumatatu katika Jarida la Tiba lijulikanalo kama Annals of Internal Medicine, kijana huyo kwa mara ya kwanza alienda kupatiwa matibabu akiwa na miaka 14 akilalamika kuwa na uchovu mwingi.

Hata hivyo, kijana huyo alikuwa hatumii dawa na alikuwa na uwiano mzuri wa uzito na kimo, hapakuwa na dalili zozote za utapiamlo  lakini madaktari waligundua kuwa ana upungufu wa vitamini B12. Hivyo walimuanzishia sindano za vitamini.

Kwa mujibu wa chuo cha Bristol mwaka mmoja baadaye kijana huyo alionesha dalili za kupoteza uwezo wa kuona na hadi kufikia miaka 17 hali ilikuwa mbaya na kufikia kupata upofu.

Wataalamu wa afya walipojiridhisha kuwa anaupungufu mkubwa wa vitamini B12 madini ya kopa, selenium na zinc nyingi sana upungufu wa vitamini D na kushuka kwa uwezo wa mifupa yake kufanya kazi.

Watafiti kutoka kitengo cha tiba pamoja na tiba ya macho kutoka chuo kikuu hicho walifanya uchunguzi na kuhitimisha kuwa  mgonjwa huyo ameathirika  mfumo wa fahamu ,pamoja na uwezo wa kuona.

Taifa Stars isibweteke bado ina kibarua kigumu
Mahakama Kuu yaitupa nje kesi ya ubunge wa Lissu