Aliyekuwa mfanyakazi wa CRDB, Gura amehukumiwa kwenda jela miaka 93 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 29 ya kughushi na 2 ya wizi wa Sh. milioni 29.8 za benki hiyo.

Aidha, mahakama hiyo imemtia hatiani Gura kwa kosa la kutakatisha Sh. milioni 29.8 na kuadhibiwa kulipa faini ya Sh. milioni 100.

Mahakama imesema akishindwa kulipa faini hiyo atakwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitano na kurejesha fedha hizo kwa benki hiyo, akishindwa kitatolewa kibali cha kufilisiwa mali zake.

Hakimu Simba amesema mahakama yake imemtia hatiani kwa makosa 32 na kwamba kosa la pili hadi la 30 mshtakiwa atakwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa.

Pia mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la 31 na 32 kwa wizi wa Sh. 29,889,191 mali ya benki ya CRDB.

Gura alidai kuwa amekaa mahabusu kwa miaka mitatu, ni mwenye familia ya mke na watoto watatu wote wadogo na wenye kumtegemea.

Hakimu Simba alisema adhabu hizo za kifungo jela zitakwenda sambamba na kwamba mahakama imezingatia maombi ya mshtakiwa.

Masoud Djuma: Lazima tuifunge Mbao FC
21 wahukumiwa kifo, kiongozi wa dini abariki