Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Fecofa), Constant Omari ameachiwa huru baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za ufisadi.

Omari alishikiliwa katika selo za Polisi akiwa na vigogo wengine watatu ambao wote kwa pamoja walihojiwa kuhusu upotevu wa $ 1 milioni, zilizopatikana kupitia mechi kubwa.

Uchunguzi unaendelea kuhusu matumizi mabaya ya ofisi na ufisadi unaodaiwa kufanyika wakati wa kuratibu mashindano ya Bara la Afrika na mashindano ya ndani ya nchi na vilabu mbalimbali.

Baada ya kutoka selo, Omari ametumia akaunti yake ya Twitter kueleza kuwa kinachofanyika kinatokana na chuki, wivu na uongo unaopikwa kummaliza.

“Shukurani zangu za dhati ni kwa vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia haki ambavyo hatimaye vimebaini kuwa huwezi kuwatuhumu maafisa kirahisi kutokana na chuki, wivu na uongo,” tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Omar.

Mbali na kuwa rais wa Fecofa, Omari pia ni mjumbe wa baraza la Fifa na makamu wa rais kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF).

Wengine waliokuwa wanahojiwa pamoja na Omari ni Katibu Mkuu wa wizara ya michezo, Barthelemy Okito na makamu wa rais wawili wa Fecofa, Roger Bondembe na Theobad Binamungu.

 

Idris 'ala shavu' Uber
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 22, 2018