Wizara ya Afya, mendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto leo Machi 31,2020 imetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid 19 Tanzania, kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo katika kituo cha matibabu ya wagonjwa walioathirika na Corona Mloganzila, Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa marehemu ni mtanzania, mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.

Wizara imetoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu na kusisitiza kuwa ” hadi kufikia leo asubuhi tarehe 31, Machi 2020 jumla ya watu waliopata maambukizi ya Covid 19 nchini ni 19, aliyepona mmoja, na kifo ni kimoja”.

Ikumbukwe kuwa jana, Machi 30 wizara ilithibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa Covid 19 baadaya kufanyiwa vipimo katika maabara kuu ya Taifa.

Taarifa hiyo imesema kuwa kati ya wagonjwa hao watatu (3) ni kutoka Dar es salaam na wawili(2) kutoka Zanzibar.

Halima Mdee: Wabunge wote tupimwe Corona
Tanzia: Katibu mkuu CUF afariki dunia

Comments

comments