Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Ilala, Dkt. Makongoro Mahanga amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Chadema wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa walipata taarifa leo asubuhi, Machi 23, 2020 kutoka kwa mke wa marehemu.

“Ni kweli taarifa hizo tumezipata kupitia Katibu wa Chadema Mkoa wa Ilala kwakuwa yeye ndiye aliyekuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu,” Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Hemedy Ally amekaririwa na Mwananchi.

“Ilikuwa twende leo asubuhi tukamuone, na taarifa zote zilikuwa zinapitia kwa Katibu wa Ilala wa chama, sasa alipofanya mawasiliano na mkewe alimwambia kuwa Mahanga ameshafariki dunia,” aliongeza.

Marehemu aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Ukonga kwa kipindi cha miaka kumi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na mwaka 2015 alihamia Chadema.

Rais wa Botswana awekwa karantini siku 14
Corona : Angela Merkel Karantini

Comments

comments