Mtoto Agnes Kiraba (3) mkazi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Kirando wilayani Nkasi amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kugongeshwa kichwa kwenye gogo na mtu anayesadikika kuwa ni mgonjwa wa akili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Justine Masejo, tukio hilo lilitokea januari 3, saa 1:30 asubuhi.

Amesema mtoto huyo alikuwa anacheza nje ya nyumba yao pamoja na watoto wenzake, ndipo alipopita mtu huyo na kumkamata kisha kumgongesha kwenye gogo.

Baada ya tukio hilo wazazi wa mtoto huyo walimkimbiza katika kituo cha afya kirando kwaajili ya matibabu lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya hali iliyo lazimu kumpa rufaa na kumpeleka kwenye hospitali ya wilaya.

Alipofikishwa katika hospitali hiyo alianza kupewa matibabu lakini alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kulalamika maumivu makali ya kichwa.

Kamanda Masejo amesema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

 

Kikongwe kizimbani kwa ubakaji
Video: Saa za meya wa Dar zahesabika, awaangukia viongozi wa dini