Serikali imesema itadhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaosafiri kwa njia ya treni, huku ikiwataka wananchi kuacha tabia ya kuwahifadhi na kuwasafirisha.

Mpango huo umebainishwa jana na naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Hamad Masauni mkoani Tabora wakati wa kikao na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo baada ya kupata taarifa za wahamiaji haramu kutumia usafiri wa treni kuingia katika mikoa mbalimbali nchini.

” Nchi yetu inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, hivyo ni vyema kudhibiti watu wanaoingia nchini pasi na kufuata utaratibu rasmi, na tuna taarifa juu ya wahamiaji kutumia njia ya treni, vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi katika maeneo husika” amesema Masauni.

Kaimu ofisa uhamiaji mkoa wa Tabora, kamishna msaidizi, Amiru Sadiki katika kikao hicho alitoa ombi kwa Serikali kuweka ma ofisa uhamiaji katika vituo vyote vya reli nchini ili kukagua wasafiri wanaoingia katika mikoa mbalimbali kama ilivyo katika viwanja vya ndege.

Awali akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama, kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, kamishna msaidizi wa polisi, Barnabas Mwakalukwa alisiema hali ni shari na kunamatukio machache ya uhalifu.

Halmashauri zatakiwa kutumia vijana kukarabati Shule
Video: Lugola abeba roho za vigogo, Chadema watoa kilio tume huru msibani

Comments

comments