Licha ya kusajiliwa kwa Thibaut Courtois akitokea Chelsea ya England kwa mkataba wa miaka sita, mlinda mlango chaguo la kwanza katika kikosi cha Real Madrid Keylor Navas ametangaza kuendelea kuwepo klabuni hapo, kwa lengo la kutetea nafasi yake.

Navas ambaye amekua muhimili mkubwa katika mafanikio ya klabu hiyo katika kipindi chote tangu alipochukua nafasi kutoka kwa aliyekua mlinga mlango wa kutumainiwa klabuni hapo Iker Casillas aliyetimkia FC Porto mwaka 2015, amesema haoni sababu ya kuondoka katika kipindi hiki ambacho anaamini kitakua sahihi kudhihirisha ubora wake.

Mlinda mlango huyo kutoka Costa Rica amesema anaamini siku zote mtu hufanikiwa anapopata changamoto ya kukabiliana na wengine, hivyo anamkaribisha kwa moyo mkunjufu Courtois, na kumtakia kila la kheri katika maisha yake mapya klabuni hapo.

“Sitohitaji kuondoka katika kipindi hiki, kwa nini niondoke? Alihoji mlinda mlango huyo baada ya kuhojiwa kuhusu hatua ya kusajiliwa kwa Courtois.

“Nipo hapa kupambana, sioni sababu ya kukimbia changamoto, nitahakiksiha ninaitetea nafasi yangu ya kuendelea kukaa langoni kama ilivyokua tangu mwaka 2015.”

Navas amekua msadaa mkubwa kwenye kikosi cha Real Madrid, baada ya kuwa miongoni mwa wachezaji waliofanikisha kutwaa ubingwa wa barani Ulaya mara tatu mfululizo.

Alijiunga na magwiji hao wa soka nchini Hispania baada ya fainali za kombe la dunia mwaka 2014, akitokea Levante, na mpaka sasa ameshaitumikia klabu hiyo ya mjini Madrid katika michezo 94.

Mafanikio mengine aliyoyapata mlinda mlango huyo akiwa na Real Madrid ni kutwaa ubingwa wa Hispania (La Liga) mara moja, UEFA Super Cups mara mbili, Supercopa de Espana na klabu bingwa duniani mara mbili.

Waliopiga Sh28.5 bilioni za Nida wachemshiwa dawa
Lucas Perez kugonga nyundo msimu ujao

Comments

comments