Mabingwa wa soka nchini England Manchester City huenda wakamkosa kiungo mshambuliaji Kevin de Bruyne kwa zaidi ya mwezi mmoja, kufuatia majeraha ya goti yanayomkabili kwa sasa.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, alipata majeraha ya goti akiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi kuu dhidi ya Huddersfield Town utakaochezwa mwishoni mwa juma hili, Etihad Stadium.

De Bruyne alianza kusumbuliwa na jeraha ya goti wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la ligi dhidi ya Everton mwaka 2016, na alikosa kucheza michezo 12 kwa kipindi hicho. Na inaripotiwa ametonesha sehemu aliyoumia tangu mwaka huo.

Mwishoni mwa juma lililopita alikua sehemu ya kikosi cha Man City, kilichochomoza na ushindi wa maboa mawili kwa sifuri dhidi ya Arsenal, akitumika kama mchezaji wa akiba.

“Muda wa kupona jeraha lake bado haujafahamika, lakini kwa taarifa za awali kutoka kwa matabibu wetu zinaeleza kuwa, huenda De Bruyne akakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja,” Imeandikwa kwenye tovuti wa klabu hiyo.

Msimu uliopoita De Bruyne alifanikiwa kufunga mabao manane na kutoa pasi za mwisho 16, na kutoa mchango wa klabu ya Man City kufikisha alama 100 kwenye msimamo wa ligi ya England, huku wakitwaa ubingwa kwa mara ya kwanza chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Hispania Pep Guardiola.

MICHEZO AMBAYO HUENDA KIUNGO HUYO ATAIKOSA.

  • Agosti 25: Wolverhampton Wanderers (Ugenini)
  • Septemba 1: Newcastle United (Nyumbani)
  • Septemba 15: Fulham (Nyumbani)
  • Septemba 18/19: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi.
  • Septemba 22: Cardiff (Ugenini)
  • Septemba 29: Brighton (Nyumbani)
  • Oktoba 2/3: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi
  • Oktoba 7: Liverpool (Ugenini)

Endapo itamchukua muda wa miezi mitatu kabla ya kurejea kikosini, De Bruyne atakosa mchezo mingine sita ambayo ni.

  • Oktoba 20: Burnley (Nyumbani)
  • Oktoba 23/24: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi
  • Oktoba 28: Tottenham (Ugenini)
  • Novemba 3: Southampton (Nyumbani)
  • Novemba 6/7: Ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya makundi
  • Novemba 11: Manchester United (Nyumbani)

RC Chalamila aamuru Jeshi la Polisi kuwasweka ndani wananchi Kijiji kizima
RC Brigedia Jenerali Nicodemas amgomea mkandarasi