Kesi ya ‘uchochezi’ inayomkabiili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe imeahirishwa mpaka Januari 29, itakapotajwa kwa ajili ya kwenda kusikilizwa.

Katika Kesi hiyo ya Jinai namba 327 ya mwaka 2018 inayomkabili Kiongozi huyo, leo katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es salaam ilitajwa kwa ajili ya kutolewa maamuzi ambayo yalitolewa na Hakimu Mkazi, Janeth Mtega baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili (Mashtaka na utetezi).

Upande wa Mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Adolf Kissima  umedai kuwa kesi hiyo leo ilikwenda kwa ajili ya kutajwa lakini upande wa mashtaka hawakuwa na jalada halisi la kesi hiyo.

Aidha, kwa upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa Zitto, Steven Mwakibolwa uliikumbusha mahakama kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na mahakama hiyo kupitia Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama, Huruma Shaidi na ilishapanga tarehe ya kuanza kusikilizwa, ambayo ni Januari 29, 2019.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT- Wazalendo, kiongozi huyo alitumia maneno yenye kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Mzimu uliomng’oa Mugabe waanza kumvuta Mnangagwa
Marekani yaionya Uturuki kuhusu Wanamgambo wa Kikurdi 'Itasimulia'