Mgombea urais wa Kenya kupitia chama tawala cha Jubilee Uhuru Kenyatta, ametaka kufutwa kwa kampeni ya kumuondoa Jaji Mkuu wa nchi hiyo David Maraga, iliyoanzishwa na mbunge wa chama hicho.

Uhuru Kenyatta amesema ni vyema kuacha Mahakama ifanye kazi zake na wao kuangalia zaidi kwenye uchaguzi wa urais unaofuatia ili kutetea nafasi ya chama hicho kubaki madarakani.

“Tumekubaliana kurudi kwa wapiga kura na masanduku ya kupigia kura, naelewa maumivu yenu na matendo yenu, lakini tuna uchaguzi wa kushinda Oktoba 17, hilo ndio linatakiwa liwe kipaumbele chetu, iacheni mahakama”, amesema Uhuru Kenyatta.

Hapo jana mbunge wa chama cha Jubilee Ngunjiri Wambugu alianzisha kampeni ya kumuondoa madarakani Jaji Mkuu wa nchi hiyo David Maraga, kutokana na kile alichokiita utendaji mbaya baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo Septemba 1 mwaka huu, na kutaka urudiwe.

Roy Hodgson amnyemelea Wilshere
Majaliwa aungana na JPM kumuombea Lissu

Comments

comments