Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri Katika hotuba yake ya kwanza katika mwaka wa 2020 aliyoitoa kwenye Ikulu ya Rais, Mombasa.

Rais Kenyatta amemteua Monica Juma kama waziri wa ulinzi huku Raychelle Omamo akiwa waziri wa mambo ya nje.

Ukur Yatani ameteuliwa kama waziri wa fedha, Mutahi Kagwe waziri wa Afya huku Betty Maina akichukua wizara ya viwanda na Sicily Kariuki akiwa waziri wa maji.

Esther Koimett waziri wa habari na mawasiliano. Simon Chelugui ni waziri wa Leba. Peter Munya ndiye Waziri wa kilimo huku Mwangi Kiunjuri akipigwa chini na wengineo pia.

Wakati wa hotuba yake Rais amesema kwamba wanaweka mipango ya kukwamua uchumi na kutoa taarifa kuwa asilimia 70 ya madeni yamelipwa.

Mkuu wa majeshi Niger afukuzwa kazi
Wanafunzi waliofanyia mtihani gerezani wafaulu kwa kishindo

Comments

comments