Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameibua mijadala nchini Kenya baada ya kuitumia sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya kumtumia salamu za heri ya sikukuu mbunge wa upinzani Millie Odhiambo ambaye mapema mwezi huu alimtolea matusi Rais huyo.

Akitumia kadi, Rais Uhuru alimjibu Millie kwa namna ambayo ilimtofautisha kabisa na Mbunge huyo na kuwa kinyume na matarajio ya wengi kuhusu hatua ambayo angechukua Rais huyo baada ya kutukanwa kwa njia ya video ambayo ilirushwa na vituo vya luninga nchini humo na kusambaa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii.

“Uhuru Kenyatta ni zaidi ya mwanasiasa,” ndiyo maneno yanayozungumzwa na Wakenya wengi kwa sasa. Huyu ndugu ametufundisha jambo kubwa la kumalizia mwaka, ni lazima tujifunze kusamehe. Huyu Mama amemtukana Rais matusi ambayo kwa tafsiri rahisi ni kama ametutukana tuliomchagua,” alisema Joseph Mwangi katika viunga vya Nairobi.

Kwa ujumla maoni ya Wa-Kenya wengi ni kuwa Mbunge huyu amemsaidia sana Rais Uhuru Kenyatta kurudi madarakani kwenye uchaguzi wa mwakani kwani wengi waliounga mkono matusi yale ni kutoka vyama vya upinzani hali inayoonyesha kuwa ni watu wanaopenda matusi badala ya upendo.

Kwa kimombo, kadi ya Rais Uhru Kenyetta iliyopambwa na picha yake akiwa na mkewe Margaret, ilikuwa na maneno yafuatayo :

“We share this holiday with all the people of all persuasions because what we celebrate are cherished universal human impulses … Often, what we see as our differences are only expressions of problems that can be resolved through a commitment to goodwill,love, peace and unity,”

Uhuru amtumia salamu za heri ya Krismasi mbunge aliyemtukana hadharani
#HapoKale