Mlinzi wa spika wa Bunge la kaunti ya Embu, Joseph Kaberia ameuawa kwa kupigwa risasi jana katika eneo la Kamiti Corner jijini Nairobi.

Kwamujibu wa duru za polisi, mlinzi huyo ambaye pia ni Afisa wa polisi alipigwa risasi kifuani na alifariki alipokuwa akipelekwa hospitali ya Ruaraka kwa matibabu.

Mlinzi huyo alikuwa na dereva wa spika kwenye gari wakati tukio hilo likitokea na wawili hao walipatikana katika eneo la mkasa baada ya wakazi kuwaita polisi waliposikia milio ya risasi majira ya saa tisa usiku.

Mkuu wa Polisi Jijini Nairobi, Philip Ndolo amesema kuwa wawili hao walikuwa wamejihami kwa bunduki dereva akiwa ametumia risasi 20 za bastola yake huku mlinzi akiwa hajatumia hata risasi moja.

Hadi sasa dereva wake amekamatwa baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa huenda anahusika kwakuwa amekutwa na majeraha ya risasi kwenye mguu wake na haijabainika jinsi alivyojeruhiwa, huku bunduki yake ikiwa imetumika risasi 20.

Hata hivyo Spika hakuwa nao wawili hao wakati tukio likitokea na Polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kisa hicho ili kubaini chanzo na  endapo bunduki ya dereva ndiyo iliyohusika kwenye mauaji hayo.

JPM aeleza sababu za kumng’oa Makamba, Simbachawene akandamizia
LIVE OLDUVAI: Maadhimisho ya miaka 60 ya kumbukizi ya ugunduzi wa fuvu la ZINJANTHROPUS BOISEI

Comments

comments