Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa kwa kitendo cha kuhudhuria kuungana na serikali katika miradi ya maendeleo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, (UDSM) ambapo amemuagiza mjumbe huyo kwenda kuwaeleza wanachama wenzie wa Chadema anao waongoza maana ya uzalendo.

“Naomba mzee Lowassa ukatusaidie kuwaelekeza na wenzako unaowaongoza huko namna ya uzalendo vinginevyo wataishia magaerezani ili wakajifunze namna ya kuziheshimu sheria za Watanzania,”amesema rais Magufuli

Hata hivyo, katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli amempongeza pia Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuanzisha wazo hilo la kujenga maktaba na yeye kuwa sehemu ya utekelezaji.

 

Mchungaji Komando Mashimo amdhamini Amber Rutty
Majaliwa aagiza kukamilika kwa wakati mradi wa maji Chato

Comments

comments