Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Kata ya Ramadhani mkoani Njombe, Robert Shejamabu amewatembelea vijana wa Chipukizi waliopo katika shule za msingi Kibena na Ramadhani Mjini Njombe kwa lengo la kuzungumza nao juu ya kujituma katika masomo yao.

Akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi Ramadhani na Kibena zilizopo katika kata ya Ramadhani Halmashauri ya mji wa Njombe, amesema kuwa wanafunzi hao wapo katika Idara ya Chipukizi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Vijana UVCCM hivyo ni jambo jema kuwa tembelea na kuwapa hamasa ili wafanye vizuri katika masomo yao.

Aidha, ametoa zawadi ya Madaftari matatu, Kalamu za Risasi mbili pamoja na kalamu za wino (Peni mbili) kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Disemba 2018 zawadi ambazo ametoa kwa washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu kuanzia darasa la awali hadi la Saba katika shule hizo mbili.

“Hata mimi nilikuwa mwanafunzi kama ninyi leo nipo hapa ni kwasababu niliamua kusoma kwa bidii jambo ambalo liliniwezesha kutimiza malengo yangu hivyo leo nimeamua kuja hapa si kwaajili ya kupoteza muda bali kwaajili ya kuwatia nguvu mkazane sana kusoma ili nanyi muweze kutimiza malengo yenu, hapa wapo wabunge, mawaziri, walimu huenda hata Rais akatoka hapa,”amesema Shejamabu

Aidha, katika ziara hiyo, kiongozi huyo aliambana na viongozi mbalimbali wa chama ambapo walipata fursa ya kuzungumza na kutoa ushauri kwa wanafunzi hao wakiwataka kusoma kwa bidii ili waendelee kufaulu vizuri katika masomo yao.

Baadhi ya walimu wa Shule ya msingi Ramadhani na Kibena wakizungumza mbele ya wanafunzi na wageni hao wamepongeza ziara hiyo ya viongozi ambao wamejitoa kuhamasisha maendeleo ya elimu katika kata ya Ramadhani huku wakiomba kuendelea kuwasaidia wanafunzi wao hasa watoto wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika Shule ya msingi Kibena ambao baadhi yao ni walemavu wa ngozi Albino

Aburuzwa kortini kwa kosa la kughushi vyeti vya taaluma
Wasichana 4000 kunufaika na mradi wa Lishe mkoani Lindi