Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Amesema kuwa anampongeza Maalim Seif kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisisa na kupigania mabadiliko ya nchi, ambapo amesema kuwa watu wengi walitegemea angepumzika na masuala ya siasa.

“Nimpongeze Maalim Seif kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani,”amesema Mashinji

Aidha, mapema hii leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.

Hata hivyo, kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.

Afariki dunia baada ya Simba kuishinda AS Vita, Simba SC yatuma salamu za pole
Polisi Kagera waua majambazi watatu

Comments

comments