Wasiwasi uliotanda ndani ya CCM kuhusu uhalali wa makada waliobaki katika chama hicho ambao walikuwa wakimuunga mkono mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa umepelekea baadhi ya makada kuanza kujitetea.

Hali hiyo ilishuhudiwa hivi karibuni kwenye mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika jimbo la Kaliua, Tabora ambapo mgombea ubunge wa jimbo hilo, Profesa Juma Kapuya alimhakikishia mgombea urais wa chama hicho, Dk John Magufuli kuwa hafanyi kazi ya kukihujumu chama kwa ajili ya Lowassa.

“Mheshimiwa Magufuli, kuna maneneo maneno ya uchonganishi hapa Kaliua kwamba mimi nampigia debe Lowassa, wanasema mchana huwa nakuwa CCM lakini usiku nakuwa Ukawa, nasema sio kweli huo ni uongo mtupu,” alijitetea Profesa Kapuya.

Alimhakikishia mwenyekiti huyo mtarajiwa wa CCM taifa kuwa yeye ni mwanachama mwaminifu na hana mpango wa kukisaliti chama hicho. Baada ya utetezi huo, Dk. Magufuli alimnadi mbele ya wananchi na kumuombea kura ili apate ushindi wa kishindo.

Edward Lowassa, alikuwa akiungwa mkono na asilimia kubwa zaidi ya wabunge wa CCM na wengi wao walionekana kuwa watiifu na marafiki wa karibu. Hivyo, baada ya kuhamia Ukawa huku wengine wakibaki katika chama hicho wameanza kunyooshewa vidole kuwa wanakihujumu chama hicho kimyakimya.

 

Chris Brown Awasha Moto Baada Ya Kukejeli Mavazi Ya Kanye West Kwa Video Hii
UEFA Kuanzisha Changamoto Mpya Kwa Vilabu