Rapper Kanye West kutoka nchini Marekani ametoa msaada wa pea za viatu vya Yeezy katika kituo kimoja cha kulelea watoto yatima kiitwacho Masulita Children’s home kilichopo wilayani Wakiso nchini Uganda.

Kanye West na familia yake walipelekwa na Helikopta binafsi kutoka Kampala hadi Wilayani Wakiso huku wakilindwa na wanajeshi kwa ajili ya usalama zaidi.

Aidha, tofauti na msaada wa viatu vinavyotengenezwa na kampuni yake, pia ametoa fedha na spika ndogo za blututh kwa ajili ya wanafunzi kusikiliza muziki na kupata burudani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho, amesema kuwa tayari wameshakubaliana kufanya ngoma ya pamoja na mwanamuziki aitwaye Bebe Cool.

Angola yawatimua wakimbizi kutoka Congo DR
Video: Mabilionea waliotekwa sehemu nyeti Afrika, 8 wang'ang'aniwa sakata la Mo Dewji

Comments

comments