Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amerejea ofisini kwake siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili ziliopita alipokuwa karantini baada ya daktari aliyempa chanjo kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona siku mbili baadaye.

Hata hivyo kwa mujiibu wa msemaji wa ofisi ya kansela Steffen Seibert, vipimo vilibaini kuwa Merkel hajaambukizwa virusi hivyo.

“Tunashukuru kuwa vipimo kadha vimeonyesha kuwa kansela bado hajaambukizwa na virusi vya Corona”, Seibert alisema huku akiongeza  kuwa, sasa ataendelea  kufanyia kazi nyumbani kwake.”

Wakati akijitenga nyumbani kwake, Merkel amekuwa akifanya mikutano ya serikali kupitia kwenye njia ya video.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za chuo kikuu cha Johns Hopkins watu wapatao 1,107 wamefariki kutokana na virusi vya Corona na wengine 84,794 kuambukizwa nchini Ujerumani.

Makamu wa Rais Zanzibar aongezewa muda wa Karantini
Video: Gongo ruksa, Wapinzani wang'aka hotuba kuzuiwa