Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewapa wiki moja Jeshi la Polisi Wilaya Bunda, kuwakamata wanafunzi watoro, wazazi wa wanafunzi watoro.

Lugola amesema kuwa inamsikitisha sana idadi kubwa ya wanafunzi wilayani humo wameacha masomo yao na kurubuniwa wanaume ili waweze  kuolewa huku Serikali ikitangaza elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mpira wa miguu wa Busambara, Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule, wilayani humo, Lugola amesema kuwa kiwango cha wanafunzi kuacha masomo inatisha,

“Mkuu wa Polisi wa hapa Bunda, nawapa wiki moja, mtumie elimu zenu za upelelezi mliofundishwa, wakamateni, wachunguzeni, wahojini ndugu,  jamaa, majirani mtawawapata wote wanaowarubuni watoto hawa, halafu mushughulike nao,” amesema Lugola.

Hata hivyo, Lugola ameongeza kuwa kuna sheria zinazoshughulika na wanafunzi watoro na pia zipo sheria zinazoshughulika na wazazi wa wanafunzi watoro, pia zipo sheria zinazowashughulikia wanaume wanaowarubuni wanafunzi.

 

De Bruyne nje miezi mitatu
IGP Sirro: Kwasasa moto wetu ni mkali