Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema kuwa taarifa zilizosambaa  kuhusu kukutwa vichwa vya watoto kituo cha polisi si za kweli na zilikuwa ni uvumi wa watu wasiokuwa na nia njema.

Ameyasema hayo jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ni watu wachache ambao waliamua kutangaza taarifa hiyo ambayo baadaye ilileta sintofahamu kwa baadhi ya wananchi wa Mwanza.

“Kuna watu walianzisha taarifa kuwa kuna watoto walikuwa wamekufa na vichwa vyao kukutwa kituo cha polisi uvumi ule uilisababisha watu zaidi ya 500 kukusanyika kuja kituo cha polisi lakini hawakuelewa, pamoja na huduma za kiusalama tunazotoa ilitulazimu tutumie mabomu ya machozi ili kuwatawanya kwa sababu waligoma kuondoka lakini pia tunawshikiria watu kadhaa kwa ajili ya mahojiano ya tukio hilo,”amesema Kamanda Murilo

Aidha, mara kwa mara kumekuwa kukiripotiwa matukio ya mauaji ya watoto katika baadhi ya mikoa nchini ambapo tayari imeshatokea katika Mkoa wa Simiyu pamoja na Njombe ambapo kupitia vyombo vya ulinzi na usalama tayari baadhi ya watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani.

Hata hivyo, mapema hivi karibuni Kamanda Jumanne Muliro alipokea kijiti cha nafasi hiyo ya Kamanda Mkoa baada ya  aliyekuwa Kamanda wa Mkoa huo Jonathan Shana kuhamishiwa makao makuu ya polisi.

Sugu matatani tena, achunguzwa kwa kosa la uchochezi
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 22, 2019