Kalonzo Musyoka amekanusha taarifa inayosambaa ikidai kuwa mwisho wa mwezi huu Februari ataapishwa na kuwa makamu wa Rais wa watu nchini Kenya.

Kalonzo amesema taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na hawezi kufanya hivyo kwa sababu ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Amesisitiza kuwa anajua Ruto anamsubiri aapishwe ili apate sababu za kumfungulia mashtaka ya uhaini na kumuharibia mipango ya kugombea urais mwaka 2022.

Amesema ”kuapishwa ni tukio la kinyume na katiba ya nchi na nasisitiza sitaapishwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari,“ Musyoka

Msyoka amezungumza hayo leo Februari 13, 2018 alipokuwa mjini Machakos akiongea na viongozi wapya walioteuliwa na NASA.

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga ajiapishe kuwa Rais wa watu nchini humo, Makamu wake , Kalonzo Musyoka hakuhudhuria siku hiyo ya kuapishwa kwake hali iliyopelekea na yeye kutokuapishwa.

Maamuzi kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi – Ligi kuu Tanzania bara
Kamati ya nidhamu yamfungia Juma Nyoso