Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Haki Elimu unaonesha kuwa fedha za ruzuku kwa ajili ya elimu bure zinazopelekwa mashuleni hazizingatii idadi ya wanafunzi kama ambavyo inapaswa kuwa jambo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu waalimu wakuu mashuleni.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kallaghe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, amesema kuwa asilimia 95 ya waalimu wakuu waliohojiwa wamekiri kuwa fedha za ruzuku wanazopata hazitoshi.
Kallaghe amesema kuwa uchambuzi wa tafiti umeonyesha kuwa baadhi ya shule zenye wanafunzi wachache zinapata fedha zaidi kuliko shule zenye zenye wanafunzi wengi hali inayoashiria kutokuwa na mpangilio mzuri wa utoaji ruzuku hiyo.
Aidha, Utafiti huo umefanyika katika Wilaya 7 zilizowakilisha kanda nchini ambazo ni Korogwe Muleba,  Tabora, Njombe, Mpwapwa, Kilosa na Sumbawanga, na kuonyesha kuwa asilimia 93 ya fedha za ruzuku zilizotarajiwa shuleni zilifika.
Hata hivyo, Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Shukio, amesema japo sera ya elimu bila malipo imesaidia kuongezeka kwa uandikishaji wanafunzi hasa wa darasa la kwanza, Serikali ichukue hatua za makusudi kushughulikia changamoto zilizopo za elimu.

Video: Mwakyembe kumbana Makonda maswali tisa, Uchaguzi wabunge AELA kaa la moto
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 6, 2017