Kaka wa Rais wa nchi ya Honduras, Juan Orlando Hernandes amekamtwa na polisi kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya, silaha na kuweka taarifa za uongo, kwa mujibu wa idara ya mahakama ya Marekani.

Mamlaka zinazohusika na kudhibiti madawa ya kulevya zilimkamata, Antonio Hernandes Alvara ambaye pia anajulikana kama, Tony Hernandes akiwa jijini Miami, lakini anashtakiwa New York nchini Marekani.

Hernandes mwenye miaka 40 ambaye pia ni mbunge, anahusika na kusafirisha tani nyingi za madawa ya kulevya aina ya cocaine yanayoingia Honduras kwa ndege, boti, na huwekwa lebo ya jina lake ya ‘TH”.

Aidha, Hernandes husafirisha madawa hayo kwa ulinzi mkubwa wenye silaha za moto, ndani ya nchi ya Honduras, akiwa na baadhi ya askari polisi wa taifa hilo la Honduras.

Hata hivyo, mwaka 2014 ilinaswa sauti yake akikutana na Davis Leonel Rivera ambaye ni kiongozi wa wafanyabiashara ya madawa ya kulevya wa Honduras, ambao wenyewe wanajiita ‘Cachiros’

Mwanaharakati wa Mazingira kutoka Tanzania kupata tuzo Ujerumani
Mhadhiri alia na rushwa ya Ngono UDSM, amtaka JPM kuingilia kati