Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini, Angellah Kairuki ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza katika sekta ya mafuta ya kula kwa kuzingatia uhitaji na soko lililopo ndani na nje ya nchi.

Amesema ni vyema watanzania wakaendelea kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la alizeti kwa kuzingatia uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula nchini kwani nchi imekuwa ikipoteza zaidi ya shilingi bilioni 443 kwa mwaka kwa kuagiza mafuta nje ya nchi.

Aidha Kairuki amebainisha kuwa uwekezaji huo ni miongoni mwa fursa muhimu na kuwataka wenye uwezo kulima zao hilo kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo kwa vile zao hilo linastawi katika ukanda huo.

Ametoa rai hiyo alipotembelea na kukagua kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula cha SUNSHINE kinachozalisha mafuta yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya alizeti, (Sunbelt) kilichopo katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma.

“Niwapongeze kwa uwekezaji mkubwa mlioufanya katika eneo hili tangu mwaka 2015 na hii inaleta chachu kwa wawekezaji wazawa kuona fursa na soko la malighafi wanazozalisha hasa zao la alizeti,” Ameeleza Waziri Kiruki

Jela miaka 7 kwa kumchoma moto mtoto
UN yamulika mauaji ya mtu mweusi Marekani