Wachezaji pamoja na viongozi wa Benchi la Ufundi wakiongozwa na Kocha mkuu Mecky Mexime jana Jumanne walianza safari  kutokea jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kujiweka fit kwa mazoezi ya  kumalizia michezo iliyobaki ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe La Shirikisho (ASFC).

Kikosi Wanankurukumbi, kinatarajiwa kuwasili katika viunga vya Manispaa ya Bukoba mjini mkoani Kagera leo Jumatano, na kitaanza maandalizi chini ya kocha mkuu, ambaye atatoa taarifa rasmi ya kuanza mazoezi.

Kocha Mexime pia atatoa utaratibu utakaotumika katika siku zote ambazo timu itakuwa mkoani Kagera, hadi taarifa rasmi ya ratiba ya ligi itakapo tolewa na mamlaka husika.

Hata hivyo kwa asilimia kubwa wachezaji wa timu hiyo wamesafiri kuelekea mkoani Kagera, japo kuna baadhi ya wachezaji ambao hawajaungana na wenzao kutokana na changamoto ya maradhi na matatizo ya kifamilia katika kipindi hiki ambacho walikuwa nyumbani.

Wakati huo huo uongozi wa Kagera Sugar, imesisitiza kuchukua hatua zote stahiki na tahadhari za awali, ili kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya Corona, ikiwemo upimwaji wa afya kwa wachezaji na viongozi wote wa benchi la ufundi mara baada ya kuwasili Mjini Bukoba mkoani Kagera.

Zlatan ajiweka pembeni AC Milan
Tetesi za usajili barani Ulaya