Serikali ya Rwanda imemuachia huru aliyekuwa mkosoaji mkuu wa Rais Paul Kagame, ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuhatarisha amani.

Victoire Ingabire, ametajwa kuwa miongoni mwa wafungwa 2,141 walioachiwa huru kupitia msamaha wa rais uliotangazwa wiki hii.

Mwanamke huyo aliyekuwa akimkosoa Rais Kagame, amekuwa akidai kupitia wawakilishi wake kuwa kifungo chake kilikuwa na shinikizo la kisiasa

Baada ya kutoka jela, Ingabire alimshukuru Rais Paul Kagame na kudai kuwa ni mwanzo mzuri wa kufungua uwanja wa siasa nchini humo.

Victoire Ingabire

Hata hivyo, Waziri wa Sheria, Johnston Businge alikanusha taarifa kuwa mwanamke huyo alifungwa kwa shinikizo la kisiasa.

“Kuachiwa kwake hakuna uhusiano wowote na siasa, na kufungwa kwake hakukuwa na uhusiano wowote na siasa,” alisema Businge.

Ingabire alikamatwa baada ya kurejea kutoka uhamishoni nchini Netherlands akiwa kwenye mpango wa kugombea urais. Alizuiwa kugombea urais kutokana na tuhuma zilizokuwa zinamkabili na baadaye alipatikana na hatia na kufungwa jela.

Kizito Mihigo

Katika hatua nyingine, jina la mwimbaji maarufu, Kizito Mihigo aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kupanga njama za kumuua Rais Kagame.

Kuachiwa huru kwa Mihigo kumekuja wiki moja baada ya kuwasilisha barua ya kuahirisha rufaa ya kupinga hukumu yake.

Pambano la Mwaka: Canelo, Golovkin kumalizana leo
CRDB kuanzisha mfumo wa kujifungulia akaunti kwa simu ya mkononi