Mwimbaji, Justine Bieber amevunja urafiki wake na bondia Floyd Mayweather wiki chache baada ya kuamua kufanya mageuzi na kumrudia Mungu akidai anataka kuishi kama mtu mwenye upako.

Bieber ambaye alikuwa mstari wa mbele kumsindikiza Mayweather kwenye pambano lake na Manny Pacquiao, ameonesha wazi kumtenga Mayweather anayesubiri pambano lake na Conor McGregor wikendi hii, kwa ku-unfollow (kumuondoa kwenye orodha ya marafiki) kwenye Instagram.

Chanzo cha karibu cha Bieber kimeiambia TMZ kuwa uamuzi wa msanii huo unatokana na ushauri anaoendelea kupewa na watalaam wa saikolojia na imani ya Kikristo

Kwa mujibu wa mtandao huo, Bieber amekuwa akishauriwa na watumishi wa kanisa la Hillsong kwa takribani mwezi sasa kujiepusha na marafiki wasio na muenendo mzuri ili kufanikisha adhma yake ya kumrudia Mungu.

Moja kati ya tabia ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha Bieber kujiepusha na Mayweather ni tabia ya bondia huyo kupenda kwenda kwenye vilabu vya usiku ambako kuna wasichana wanaocheza wakiwa watupu (strip clubs).

Vyanzo hivyo, vimedai kuwa Mayweather ameshangazwa na kitendo cha Bieber na kudai kuwa amekuwa msaliti kwake.

Aubameyang Apinga Msimamo Wa Borussia Dortmund
Ali Kiba aliamsha dude, anamkejeli Diamond ‘Malkia wangu wa Nguvu...’