Justin Bieber anaumaliza mwaka 2018 kwa kupambana na changamoto ya kukosolewa vikali mitandaoni baada ya kuandika ujumbe ambao haukuwafurahisha wengi dhidi ya ‘post’ ya mtoto wa miaka 15.

Mtoto Jojo Siwa aliweka kwenye Instagram picha inayoonesha zawadi ya Krismas aliyopewa, ambayo ni gari aina ya BMW lenye picha yake na maandishi, “Nickelodeon’s JoJo Siwa D.R.E.A.M. The Tour.”

Jojo ambaye ni mwanamuzi aliyetoa albam ya D.R.E.A.M, muigizaji na mtu maarufu kwenye YouTube alionekana kuipenda zaidi zawadi yake lakini Justine Bieber alikuwa na maoni tofauti yaliyouchoma moyo wake.

Bieber alijitokeza kwenye picha hiyo na kuandika “Burn It” (ichome). Kwa msisitizo, mkali huyo wa Sorry aliandika ujumbe huo mara tatu.

Mashabiki wa Jojo hawakupenda na waliamua kuandika jumbe kali za kumkosoa kwa kile walichodai amemnyanyasa mtoto huyo.

  • Dkt. Bashiru akemea rushwa ndani ya CCM

Mama yake Jojo, Jessalynn Siwa naye aliingilia kati akimtetea mwanaye kwa kumjibu Bieber, “Burn your own things” yaani choma vitu vyako mwenyewe.

Baada ya vita ya maneno na ‘meme’ kadhaa, Justin Bieber alilazimika kujibu kwa kujieleza kuwa hakuwa na tatizo na Jojo bali hakupenda rangi za gari alilopewa.

“Sina tatizo lolote na Jojo, sikupenda tu rangi za gari lake na mimi ninaamini hamkuichukulia kama ugomvi au vinginevyo,” tafsiri isiyo rasmi ya alichokiandika Bieber.

Makala: Wateule watano wa JPM ‘waliokiki’ zaidi 2018 na mambo yao
Chama tawala chashinda uchaguzi kwa kishindo

Comments

comments