Mwigizaji wa tamthilia ya Empire Jussie Smollet anaetambulika kama Jamal katika tamthilia hiyo amejipalia kaa la moto baada ya kutuma barua kwenye kampuni ya FOX ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa mapenzi ya jinsia moja  kwa kampuni ya FOX studio anayofanya nayo kazi siku moja kabla ya shambulio

Jussie alijisalimisha mikononi mwa Polisi siku ya Feb 21,2019  ili kusikiliza mashtaka yake ya kuwadanganya Polisi kuhusu kutekwa Chicago.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwigizaji huyo ana nafasi ndogo ya kushiriki katika msimu mpya wa tamthiliya ya Empire ambayo inatajwa kuonyeshwa mwaka 2020 baada ya FOX kutangaza rasmi msimu ujao wa Empire.

Mtandao wa televisheni ya FOX umetangaza kuwa msimu wa sita ndio utakua wa mwisho wa tamthiliya hiyo ya Empire na inapanga kufanya onyesho kubwa la televisheni

Aidha  mtendaji mkuu wa mtandao huo Charlie Collier alisema kuwa kuhusu Jussie Smollet hawana mpango wa kumjibu chochote ikiwa baadhi ya sehemu zake ndani ya tamthiliya hiyo  zimeonekana kumalizika.

Marekani yadai haitaki vita na Iran
Mfalme Mswati akanusha wanaume kuoa wanawake wengi au kifungo jela

Comments

comments