Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, Lucas Nyanda amempongeza Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama hicho, Neema Mgaya kwa kuchangia ujenzi wa jengo la CCM mkoa wa Njombe zaidi ya milioni saba.
Nyanda alitoa pongezi hizo wakati akizumgumza na Dar24 ambapo amesema kuwa kwa ofisi ya Jumuiya ya Wazazi pekee amechangia zaidi ya laki tano mpaka kukamilika kwake.
“Kiukweli Mh. Neema anatakiwa kupewa pongezi za kipekee kwani ndio Mbunge pekee kwa mkoa wa Njombe ambaye amechangia kiasi kikubwa katika ujenzi wa jengo hili” amesema Nyanda.
Kwa upande wa Mbunge huyo wa Viti Maalumu Mkoani Njombe, Neema Magaya amesema amechangia jengo hilo ili liweze kukamilika kwa wakati pamoja na kuharakisha shughuli za chama.
Mnyika amshukuru JPM, 'Watanzania wanakuombea usiwe na kiburi'
Video: Kubenea amfungukia JPM,'Nakuunga mkono kwa asilimia 200%'

Comments

comments