Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Colombia Juan Cuadrado ameafiki kumuachia jezi namba saba mshambuliaji mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye wakati wowote atatambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari.

Ronaldo amezua gumzo zito kwenye vyombo vya habari tangu mwanzoni mwa wiki hii, kufuatia uhamisho wake wa kutoka Real Madrid kwenda kwa mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus kwa zaidi ya Euro milioni 80.

Mshambuliaji huyo amekuwa shabiki mkubwa wa jezi namba saba (7) tangu akiwa na klabu ya Manchester United ya Uingereza, hali ambayo imetoa msukumo kwa uongozi wa Juventus kumuomba Cuadrado kuiacha namba hiyo ya jezi, ili apatiwe mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno.

Cuadrado amekubali ombi la uongozi wa Juventus na tayari ameshathibitisha katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuandika: “Ni bora kutoa kuliko kupokea. Nimekubali na ninamtakia kila la kheri.”

Image result for Cuadrado has given up his Juventus Number 7 jersey for new arrival Cristiano Ronaldo

Hatua ya kukubali kwa kiungo huyo ambaye alikuwa sehemu ya kiosi cha Colombia kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi, kunatajwa kurahisisha kazi kwa uongozi wa Juventus ya kumtambulisha Ronaldo katika vyombo vya habari.

Kazi nyingine iliyorahisishwa kufuatia kukubali kwa Cuadrado, ni kuchapisha kwa wingi jezi namba saba za klabu ya Juventus zitakazokuwa na jina la Ronaldo kwa ajili ya kuuzwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.

EXCLUSIVE VIDEO: Uhamiaji wataja mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu 'PASSPORT'
Kisa cha mwanamke aliyekataa kuolewa na mwanaume aliyemtolea figo