Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa anajua wapo watakaotumika kuleta vikwazo kwenye hatua anazopiga za kuiletea maendeleo nchi.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa jengo la PSPF mkoani Dodoma, ambapo Rais Dkt. Magufuli amesema kwamba wapo ambao hawapendi kuona Tanzania inapiga hatua kwenye uchumi, hivyo watu watatumika na mabeberu kuleta vipingamizi na vikwazo, lakini yeye ataendelea kuchapa kazi kwa ajili ya watanzania masikini.

“Katika juhudi hizi za kuleta maendeleo wapo wengine watasaliti njiani, wapo wengine watatumika na mbinu za mabeberu, na hasa katika masuala haya ya kujenga nchi yetu, na hasa kwa sababu nchi yetu inakwenda mbele, ni lazima itawakwaza wengine, katika jukumu lolote la kazi hata kwenye familia, lazima watapatikana wa kupinga pinga kidogo, lakini kikubwa ni kunyoosha mstari kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania masikini”, amesema Rais Dkt. Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amemuhakikishia mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, Makongoro Nyerere, kuwa nchi ipo salama na imara, na anaamini itafika ikiwa imara zaidi licha ya vikwazo vingi anavyokutana navyo.

Usambazaji wa gesi ya bei nafuu kuanza jijini Dar
Makonda aifanikisha safari ya mwisho ya Masogange