Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa ni lazima kila mtu afanye kazi ili aweze kuishi maisha mazuri.

Ameyasema hayo mapema hii leo wilayani Chato mkoa wa Geita wakati wa uzinduzi wa tawi la benki ya CRDB, ambapo amesema kuwa yeye si mwanasiasa ambaye anatumia maneno ya uongo.

Amesema kuwa ataendelea kuongea ukweli hivyo watu watakaoendelea kuchukia kuambiwa ukweli waendelee kumchukia lakini ukweli wataupata.

“Mimi kila siku huwa napenda kusema ukweli, anayechukia ukweli acha aendelee tu kuchukia, mtu asiyefanya kazi bora afe tu,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, ameipongeza Bodi na uongozi mzima wa CRDB kwa kufungua tawi wilayani Chato na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Waandishi wa habari 25 watupwa jela
Makonda kuwanyoosha wanaume wa Dar wanaokimbia mimba zao