Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya viongozi wa serikali wanaotaka kugombea Ubunge.

Aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wabunge wa chama hicho siku kadhaa zilizopita, katika video iliyosambazwa mitandaoni na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, ambapo Rais Magufuli amesema kuwa lazima watu waridhike kwani hawawezi kuwa na vyote.

”Hao wanaojipanga kugombea uchaguzi ujao wakiwemo wakurugenzi, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nyie waacheni tu, wakagombee nyie fanyeni kazi, kuna watu wanatamaa sana,”amesema Rais Magufuli.

Aidha, akitolea mfano wa baadhi ya viongozi waliowahi kutumikia nyadhifa za ukuu wa mkoa na wilaya na baadaye kugombea nafasi za ubunge, Rais Magufuli amesema kuwa sio kwamba hawaoni au hawafahamu bali ameona wanatamaa na hawamfai katika serikali yake.

 

Video: Hoja ya Msukuma kwa Bongo Movie ni shuti, ya Zamaradi na Steve Nyerere..! (Makala)
Kilio cha wasanii chasikika, Majaliwa achukua maamuzi magumu

Comments

comments