Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewateua Waziri Mkuu Mstaafu, Kayanza Mizengo Peter Pinda na Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa Halmashuri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Aidha, rais Dkt. Magufuli amefanya uteuzi huo kwa kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa katiba ya CCM toleo la mwaka 2017.

Majina ya wateule hao yatawasilishwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika siku zijazo jijini Dar es salaam

Video: Hoja ya Nape yamliza Waziri kama mtoto, Kiama waliotajwa mali za CCM kuanza Jumatatu
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 25, 2018