Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewazadia viwanja wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki katika mashindano ya Mataifa Huru Barani Afrika (AFCON).

Ametoa zawadi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji hao mara baada ya hapo jana kufanikiwa kuifunga magoli 3- 0 timu ya taifa ya Uganda (Uganda Craine)

Amewapongeza wachezaji hao kwa mchezo mzuri waliouonyesha hapo jana na kuwataka kuongeza juhudi kwani mchezo wa mpira wa miguu ni biashara hivyo hawapaswi kuitelekeza sababu inasaidia kukuza uchumi.

”Leo nimewaita hapa kuja kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya hapo jana, ninakuwaga ni mgumu sana kutoa pongezi lakini leo imenibidi niwapongeze, kwa hili mlilolifanya jana, ninatoa zawadi ya kiwanja kwa kila mmoja, Dodoma, Waziri mkuu simamia hili,”amesema JPM

Aidha, katika hatua nyingine Rais Magufuli amempatia kiasi cha shilingi milioni tano mchezaji wa zamani wa taifa stars, Peter Tino mara baada ya kumuomba kusalimia viongozi mbalimbali waliokuwa wamehudhuria katika hafla hiyo.

Pia Rais Magufuli amempongeza bondia Hassani Mwakinyo na kumpatia zawadi ya kiwanja mkoani Dodoma mara baada ya kufanya vizuri katika pambano lake lililofanyika jijini Nairobi nchini Kenya, ambapo alimchakaza bondia kutoka nchini Argentina, Sergio Gonzalez.

Hata hivyo, timu ya taifa (Taifa Stars) hapo jana ilifanikiwa kutinga katika fainali za mataifa huru barani Afrika (AFCON) baada ya miaka 39 kupita bila kufanikiwa kushiriki katika mashindano hayo.

Cardi B amburuza mwandishi mahakamani
Serikali ya Dubai yamkana R Kelly

Comments

comments